Arsenal yarejea kileleni ikimchezesha mtoto wa miaka 15, na kuvunja rekodi ya EPL

 


Arsenal imerejea kileleni mwa ligi kuu England baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Brentford.

Mabao ya William Saliba, Gabriel Jesus na Fabio Vieira yalitosha kuipa alama 3 Arsenal na kufikisha 18, moja zaidi ya Manchester City walio katika nafasi ya pili.

Katika mchezo huo, kijana mdogo Ethan Nwaneri, mwenye umri wa miaka 15 aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza ligi kuu England(EPL)

Mwanafunzi huo aliingia dakika za majeruhi kuchukua nafasi ya Fabio Vieira na angalau aligusa mpira mara moja.

Kinda huyo aliitwa tu kwa mazoezi ya kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza siku ya jana, hasa baada ya kukosekana kwa nahodha Martin Odergaad aliye majeruhi.

Kocha Mikel Arteta akavutiwa naye na leo kampa nafasi. Ethan alizaliwa mwaka 2007, ambapo uwanja wa Emirates unaotumiwa na Arsenal ulifunguliwa kabla hajazaliwa!

Post a Comment

0 Comments