Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Anthony
Sinare leo Septemba 28, 2022, ameongoza kikao baina ya BRELA na COSOTA
kilichokuwa kinajadili kuhusu mchakato wa kuanzisha kituo cha kutoa elimu ya
Miliki bunifu kwa wadau wa hapa nchini Tanzania ambacho kitafadhiliwa na
Shirika la Kimataifa Duniani la Milki Bunifu (WIPO).
Akizungumza katika kikao hicho Doreen alieleza maelekezo ya WIPO kwa hatua za
awali za utekelezaji ni kujaza taarifa za msingi za utekelezaji wa mafunzo hayo
(training need assesment) na taarifa hizo zitahitajika kujazwa na COSOTA,
BRELA, ZBPRA na COSOZA.
Akifafanua kuhusu umuhimu wa kushirikisha Taasisi hizo Msimamizi huyo wa
Hakimiliki Tanzania alisema COSOTA na COSOZA ni Ofisi zinazosimamia masuala ya
Hakimiliki (Copyright) na BRELA na ZBPRA zinasimamia ubunifu unaohusisha mali
viwanda (Interlectual Property) na Kimataifa Taasisi hizo ni wanachama wa WIPO,
hivyo ni vyema kushirikiana ili kila mmoja aweze kunufaika na fursa hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Bunifu
kutoka BRELA Seka Kasera alishauri kikao cha kuzungumzia jambo hilo kufanyika
ndani ya mwezi Oktoba 2022, lengo nikuhakikisha mchakato huo unakamilika haraka
ambapo, madodoso hayo ya taarifa za msingi ya kuanzishwa kwa kituo hicho ni
vyema yakawasilishwa kwa wataalamu wa Ofisi ya COSOZA na ZBPRA ili katika kikao
hicho kila mmoja awe na uelewa na kutoa ushauri wa moja kwa moja kurahisisha
mchakato.
"Pia katika kikao hicho ni vyema Wanasheria wa kutoka na COSOTA na BRELA
pamoja na COSOZA na ZBPRA za Zanzibar kuja na rasimu ya mkataba wa makubaliano
ya kuanzisha kituo hicho nchini na WIPO (MoU).
0 Comments