Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi leo amefanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura ambapo amesema amekuwa akipata Ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi.
IGP Wambura alimweleza Rais Mwinyi kuwa Jeshi hilo litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ikiwemo kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuipa kipaumbele Kamisheni ya Polisi Zanzibar kutokana na mazingira yake katika suala zima la usalama.
Lengo la Ziara ya IGP Wambura ni kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
0 Comments