Serikali imesema suala la haki ya faragha kwa Wafungwa na Wenza wao itaanza kutolewa pale ambapo mifumo ya kisheria na miundombinu ya Magereza itakapokidhi kutolewa kwa haki hiyo.
Kauli hiyo imetolewa bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni alipokuwa akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji wakati ambao wafungwa watapata haki hiyo.
Waziri Masauni amesema masuala mengine yatakayozingatiwa kabla ya kuruhusiwa ni usalama, mila na desturi za Tanzania kwani haki hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa faragha.
Aidha amesema serikali inaendelea kutoa haki nyingine za msingi kwa wafungwa ikiwemo malazi, mavazi na chakula
“Tendo la ndoa ni haki lakini sio haki ya msingi, haki ya msingi ambayo tunatoa kwa wafungwa ni chakula, mavazi, malazi. Kuna mambo mengi ambayo yanapaswa kufanyika kwanza kabla ya kuruhusu haki hiyo gerezani,” amesisitiza Waziri Masauni
0 Comments