Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa saratani
umeua watu 25,000 mwaka 2020 na kuufanya ugonjwa huo kuwa tishio zaidi ya
Uviko-19 iliyoua watu chini ya 1,000 hapa nchini.
Waziri Ummy amesema Serikali imeiomba jumuiya ya kimataifa kushiriki katika
mapambano ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni miongoni mwa hatua ambazo
zimechukuliwa kukabili ugonjwa huo.
Waziri Ummy amesema hayo leo Jumatatu Septemba 26, 2022 jijini Dar es Salaam
katika uzinduzi wa taarifa ya Taasisi ya The Lancert Oncology ya hali ya
ugonjwa wa saratani katika nchi zilizo usini mwa Jangwa la Sahara kwa upande wa
Afrika Mashariki.
Waziri Ummy amesema "Tutaendelea kutoa chanjo ya Saratani nchini ili kuhakikisha tunawekeza katika huduma za kinga, kwa kuendelea kutoa elimu kwa watanzania jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa saratani.
0 Comments