Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
amewasili jijini London, Uingereza kwa ajili ya kushiriki shughuli rasmi ya
msiba wa Malkia Elizabeth II.
Viongozi mbalimbali walioalikwa akiwemo Rais Samia watatoa
heshima zao za mwisho kwa Marehemu kwenye eneo la Westminster Hall ambapo pia
atatia saini kitabu cha maombolezo.
Baada ya hatua hiyo Rais Samia atahudhuria hafla fupi
ilioandaliwa Mfalme Charles III ambaye amemrithi mama yake Marehemu Malkia
Elizabeth II.
Hafla hiyo ambayo pia imeandaliwa na Malkia Mfariji (Queen
Consort), Camilla Parker Bowles itafanyika katika Kasri ya Buckingham jijini
London.
Aidha, siku ya Jumatatu, Rais Samia atahudhuria Mazishi ya
Kitaifa ya Malkia Elizabeth II yatakayofanyika kwenye Kanisa la Westminster
Abbey, Mwili wa Malkia Elizabeth utalazwa kwenye kasri la Windsor.
0 Comments