Rais wa Kenya William Ruto amesema katika utawala wake
hatamteua mwanachama yeyote wa upinzani kwa kuwa hali hiyo itadhoofisha
Upinzani.
Akizungumza mjini Naivasha katika mkutano wa kundi la
wabunge wa Kenya Kwanza, rais alisisitiza kwamba anataka chama cha upinzani
chenye nguvu ambacho kitasaidia kuhakikisha serikali yake inafanya kazi kwa
uthabiti.
Ruto alisema upinzani mkali, unaweza kuendesha serikali
inayowajibika.
“Hatutamteua mwanachama yeyote wa upinzani kwa sababu
tunataka upinzani mkali, tunataka upinzani ambao utaiweka serikali kwenye
udhibiti Mkali. Tunataka kuendesha serikali inayowajibika; hatuna cha kuficha,”
alisema.
Kwa upande wa kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga amewakosoa Majaji wa Mahakama ya Juu kuhusu jinsi walivyoshughulikia kesi ya uchaguzi wa urais wa 2022.
Akiongea mjini Machakos Ijumaa, Septemba 16, wakati wa
mkutano wa viongozi waliochaguliwa Azimio, alisema kuwa, majaji wa Mahakama ya
Juu, walijazwa chuki.
Aliendelea na mashambulizi yake makali dhidi ya Jaji Mkuu
Martha Koome, akimshutumu kwa kutumia lugha ya kudhalilisha katika uamuzi
ulioidhinisha ushindi wa William Ruto.
“Wakati wowote majaji wanapotumia maneno makali kwa
mawakili, ni matokeo ya kuvurugika fahamu. Mahakama Kuu sasa iko kwenye siasa.
Mimi naamini uamuzi huo uliongozwa na shetani,” alisema.
0 Comments