Uwanja wa Kasarani ambako sherehe ya kumuapisha rais wa tano wa Kenya William Ruto inafanyika leo umejaa .
Wakenya kutoka sehemu mbali mbali za taifa walianza kufurika uwanja huo alfajiri na kufikia saa kumi na moja asubuhi hapakuwa na nafasi ya watu zaidi kuingia uwanjani.
Tayari polisi kupitia msemaji wa huduma hiyo Bruno Shioso wamewashauri wananchi kuifuatilia hafla hiyo majumbani mwao .
0 Comments