Watumishi Wa Tume Ya Ualimu Watakiwa Kufuata Miongozo Na Kanuni.

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mhe Innocent Bashungwa amewaagiza watumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu nchini kufuata miongozo, kanuni za kiutendaji pamoja na kutimiza majukumu yao kwa ufasaha ili kusaidia kutimiza azma ya Serikali katika kuimarisha tume ya Utumishi wa walimu pamoja na kada ya ualimu.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa Kamishna mpya wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Felister Shuli ambae anachukua nafasi ya Mathew Kirama.

Bashungwa amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia ni kuimarisha Tume ya Utumishi wa Walimu hivyo tunategemea tukio hili litaimarisha umoja na kuwa chachu ya kutimiza majukumu yenu ya kumsaidia Rais Samia katika kuwahudumia walimu katika kupata sitahiki zao na kutimiza majukumu yenu kwa ufasaha”

Aidha Bashungwa amemtaka Kamishna huyo kutumia uzoefu na weledi alionao katika kutetea maslahi na stahiki za walimu nchini ili watumishi hao waweze kutimiza majukumu yao bila vikwazo.

“Unakwenda kuungana na wajumbe wengine, una uzoefu wa kutosha kwa hiyo nenda ukatumie uzoefu ulionao katika kutetea maslahi na stahiki za walimu ili kuleta matokeo chanya” ameongeza Bashungwa


Post a Comment

0 Comments