Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,
linamewakamata watuhumiwa wawili kwa makosa ya kimtandao kufuatia msako mkali
unaoendelea unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kikosi kazi
maalum cha kupambana na makosa ya kimtandao.
Mtuhumiwa wa kwanza ni Innocent Adam Chengula, Mhehe, 23, mkazi wa Kigogo
Luanga, amekamatwa kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Dkt. HASSAN ABBAS
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu kupitia mtandao na kutumia laini za simu zenye usajili usio na
majina yake.
Mtuhumiwa huyu amekuwa akiweka picha na majina ya Dkt. Hassan Abbas katika
maelezo ya ukurasa wake mitandaoni ya kijamii (Profile) na kutuma jumbe kwa
watu akiwaomba wamtumie fedha kwenye namba tofauti za simu.
Mfano Amekuwa akituma jumbe zinazosomeka
“kaka naomba niazime millioni 3 alhamis nitakurudishia”
na nyingine
“kaka nina mtoto wangu naomba umpatie kazi apo kwako yeye amesomea bachelor of commerce in accounting”.
0 Comments