"Kikosi chetu kimerejea rasmi mazoezini baada ya juzi
kurejea kutokea Angola. Kilianza mazoezi jana asubuhi kwenye uwanja wetu wa Mo
Simba Arena na leo kitaingia kambini."
"Tulishinda lakini bado hatujafuzu, safari hii hatutaki kurudia makosa.
Tumeweka nguvu kubwa kuona kwamba mchezo wa jumapili tunapata matokeo mazuri
ili tuingie makundi. Tumemiss kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika."
"Tutaendelea kuwakosa Shomari Kapombe ambaye sasa anaendelea kufanya
mazoezi akiwa hospitali, ataukosa mchezo wa jumapili lakini michezo itakayofata
atakuwepo. Jimmyson Mwinuke pia tutamkosa, taarifa njema ni Peter Banda
amerejea kikosini."
"Wageni wetu Primeiro de Agosto watawasili nchini Oktoba 14 majira ya
mchana, kwa wale ambao wangependa kwenda kuwapokea wanakaribishwa uwanja wa
ndege. Waamuzi wanatokea Afrika Kusini na watawasili nchini siku hiyo hiyo ya
Oktoba 14."
"Upande wa hamasa tunaendelea kupita kwenye vyombo vya habari na kupita
mitaani, siku ya ijumaa tutakuwa Temeke, tutazunguka na kispika twende
tukaiunge mkono timu yetu. Tukio la kipekee tutakuwa na chakula cha pamoja,
biryan la kwenda hatua ya makundi."- Ahmed Ally.
0 Comments