Bil.69 Zatengwa Kwaajili Ya Ununuzi Wa Vifaa Tiba



Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali kupitia Ofisi ya Rais-Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa imetenga fedha kiasi cha shilingi Bil. 69.65 kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba vitakavyosambazwa katika vituo vya afya nchini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya nchini.

Hayo yamesemwa Bungeni Novemba 9, 2022 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Festo Dugange wakati wa kujibu swali la Eng. Ezra Chewelesa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mangharibi.

Katika swali lake la Msingi Mhe. Chewelesa alitaka kujua ni lini vituo vya Afya vya Lukaragata na Nemba vilivypo katika Halmashauri ya Biharamulo vitapewa vifaa vya upasuaji.


Akijibu swali hilo Mhe. Dugange amesema kuwa kiasi Sh. Bil. 69.65 zimetengwa kwaajili ya kununua vifaa tiba, kati ya fedha hizo Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo imetengewa Mil. 250 kwaajili ya ununuzi wa vifaa hivyo.

Aidha katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilipeleka vifaa vya upasuaji ikiwemo kitandaa, taa ya upasuaji pamoja na mashine ya X-ray katika kituo cha afya Nemba.

Dugange amesema kuwa kwakuwa Kituo cha Afya Lukaragata bado hakina chumba cha upasuaji, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo itatenga fedha kiasi cha Sh. Mil 50 katika Mwaka wa fedha 2023/2024 kwaajili ya kuanza ujenzi wa jengo la X-ray ili huduma hiyo ianze kutolewa . 


Post a Comment

0 Comments