Kamishna Jenerali Lyimo, Balozi Dk.Bana Wafanya Mazungumzo Nchini Nigeria.

KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk. Benson Bana.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Septemba 25, 2023 Kamishna Jenerali Lyimo na Balozi Dk.Bana wamejadili kwa kina kuhusu namna bora ya kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya kati ya Tanzania na nchi za Afrika Magharibi.

Balozi Dk. Bana, pia anawakilisha nchi 14 zilizopo ukanda magharibi mwa Bara la Afrika.Nchi hizo ni Mali, Togo, Ghana , Guinea-Bissau, Guinea, Mauritania, Niger, Cote d' Ivoire, Burkina faso, Gambia, Senegal, Liberia, Bennin , na Siera Leon,

Kamishna Jenerali ambaye ameambata na ujumbe kutoka Tanzania, nchini Nigeria kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya kwa Nchi za Afrika HONLEA AFRICA 31, ambao unafanyika kuanzia Septemba 25 hadi 29 Septemba 2023 jijini Abuja.

Tanzania iliwahi kuwa mwenyeji wa Mkutano HONOLEA AFRICA 28 Mwaka 2018 mwezi Septemba.



Post a Comment

0 Comments