Kikosi hicho kimeingia kambini baada ya mapumziko ya siku moja tangu kipocheza mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union Alhamisi (Septemba 21) na kushinda mabao 3-0.
Kocha Mkuu Robertinho amesema wameanza rasmi kujiandaa na mchezo dhidi ya Power Dynamos na mazoezi yao yote ni kuelekea kwenye mchezo huo muhimu ambao wanahitaji ushindi tu.
“Tumeanza na programu Maalum kwa wachezaji wote kwa kuvigawa katika makundi mawili, lakini kiujumla tumeanza kujiandaa na mchezo wetu wa mrudiano, tunataka kuona tunaingia hatua yÃ¥ makundi,” amesema Robertinho.
Aidha, amesema wapinzani wao si timu dhaifu na watakuja kwa nguvu kujaribu kulazimisha ushindi au sare yenye manufaa kwao.
“Mchezo hautakuwa mwepesi, lakini nina imani na wachezaji wangu ingawa nitamkosa Inonga (Henock), lakini waliobaki wanaweza wakanipa kile ambacho nakitaka na mashabiki wanachokisubiria” amesema Robertinho.
Inonga ataukosa mchezo huo baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal union na anatarajiwa kuwa nje kwa majuma mawili.
0 Comments