DCEA Yasaini Mkataba Wa Ushirikiano Kudhibiti Uchepushwaji Kemikali Bashirifu.


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) imesaini mkataba wa ushirikiano katika udhibiti wa uchepushwaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya na Mamlaka ya Maabara ya Kemikali ya Serikali @gcla_official Mamlaka ya dawa na Vifaa Tiba ya Tanzania @tmda_tanzania , Baraza la Famasi la Bohari Kuu ya Dawa @msdtanzania na wawakilishi kutoka sekta binafsi katika viwanda vya kemikali na dawa tiba zenye asili ya kulevya.


Shughuli hiyo ya utiaji saini imefanyika leo tarehe 16 Oktoba 2023 katika ukumbi wa mikutano wa kituo cha utalii cha Ngorongoro jijini Arusha.



Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo Kamishna Jenerali wa @dceatanzania Aretas Lyimo amesema kichocheo kikuu cha kuimarisha juhudi hizi za pamoja kupitia Mkataba huo wa ushirikiano ni uwepo wa viashiria vinavyoonyesha ongezeko la biashara haramu ya kemikali hatari na matumizi yake katika uzalishaji wa dawa ya kulevya na dawa mbadala ya kulevya.

#Jmtzmedia #WatchYourWord



Post a Comment

0 Comments