Wanafunzi acheni matumizi ya simu shuleni – ACP Mallya

 


Wanafunzi katika ngazi tofauti, wametakiwa kuachana na matumizi ya Simu za mkononi na mitandao ya kijamii, ili kuepukana na wimbi la mmomonyoko wa maadili katika makuzi yao na kupelekea kupoteza malengo kwenye masomo.

Wito huo, umetolewa Oktoba 16, 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya, wakati akiongea na Wanafunzi wa wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Oswe na kuongeza kuwa jamii ina changamoto hasa kwenye suala la malezi, ambalo limepelekea watoto wengi kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa.

Amesema, Wanafunzi hao pia wanatakiwa kuchagua aina ya marafiki ambao watakuwa kimbilio kwao na msaada katika makuzi yao na kwamba, kujihusisha na makundi ya marafiki usiofaa ni chanzo cha kupoteza dira maishani, kwani itapelekea kuharibu ndoto zao kiujumla.

Kuhusu Walimu, Kamanda Mallya aliwataka waendelee kuwajenga Wanafunzi hao kwa kuwafundisha mambo mbalimbali ikiwemo athari za matumizi ya Dawa za kulevya, kujihusisha kimapenzi katika umri mdogo na kutambua haki na wajibu wao.

Post a Comment

0 Comments