DAR ES SALAAM: HOSPITALI ya Taifa Muhimbili leo imezindua mtambo wa Hyperbaric Medicine unaotibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia asilimia 100 ya hewa tiba mgandamizo ya oksijeni.- Mtambo ambao ni wa kwanza kwa Afrika Mashariki na wapili kwa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara - Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa Hyperbaric Medicine kutoka Muhimbili, Dk Albert Magohe na kusema kuwa mtambo huo unatibu magonjwa mengi ambayo hayakuwezekana kutibiwa nchini hapo awali. - "Mtambo huu husaidia matibabu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo madonda sugu yatokanayo na kisukari, maambukizi ya kwenye mifupa, waliopata madhila ya matibabu ya mionzi, waliopoteza uwezo wa kusikia, walioungua kwa muda mrefu, wale wenye upotevu mkubwa wa damu na kutokana na hali zao hawatakiwi kuongezewa damu, - "Pia hutibu waliopata madhara ya bahari yanayoweza kupelekea kiharusi kwa mgonjwa 'Decompression sickness' kutokana na uvuvi au utalii wa kuzamia chini ya maji," amesema Dk Magohe. - Akizungumzia gharama za mtambo huo Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema mtambo huo umetengenezwa na Kampuni ya Sechristl na umegharimu Sh milioni 250.
0 Comments