Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally @ahmedally_ amesema Mashabiki wa Simba SC siku ya Jumanne ya Wiki ijayo watafanya kazi nusu siku na ikifika saa sita watafunga ofisini na kwenye uwanjani kuishangilia Timu yao kwenye mechi dhidhi ya Wydad.
Akiongea leo Jijini Dar ea salaam, Ahmed amesema “Jamhuri ya Simba tunaitangaza siku ya Jumanne kufanya kazi ni nusu siku, ikifika saa 6 tunafunga ofisi baada ya hapo tunakwenda uwanjani na kama una Boss muombe ruhusa mapema, kama Boss ni Mtata tuwasiliane ili tuongee nae, Jumanne itakuwa ni Mnyama Tuesday, Half Day”
“Nawahakikishia tutaingia robo fainali na Jumanne tutaanza kuonesha hilo lakini ili tufanikiwe ni lazima kila Mwanasimba kushiriki kuja uwanjani, mechi ya Kagera Sugar ni maandalizi ya mechi dhidi ya Wydad na tiketi zake zitaanza kuuzwa kesho, mechi dhidi ya Wydad itakuwa December 19, 2023 saa 10:00 jioni na tutaingia tukiwa na option moja tu, kushinda, tutaweka rehani roho zetu ili kushinda”
“Wydad watakutana na moto wa volcano, siku hiyo lazima wakae na tushinde, mechi hiyo inawahitaji zaidi Wanasimba ni mechi ya kutengeneza njia ya kwenda robo fainali, Simba sio timu ya kuishia hatua ya makundi”
“Mgeni rasmi atakuwa Mwalimu Abdelhak Benchikha ‘GENERAL’, yeye ndio tumempa hadhi hiyo, huyu ndio Kocha bora wa Afrika kwa vilabu na Kocha wa tatu kwa ubora Afrika lakini pia ni mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika tukiwa nyumbani na sababu kuu ni mabadiliko ambayo ameyaleta, huyu ni Kocha mkubwa sana Afrika, Wanasimba tujivunie tukiwa ba kocha Abdelhak Benchikha, Ndugu yangu Mwanasimba na wewe hakikisha unaandika historia siku hiyo kuwepo uwanjani”
0 Comments