Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inashiriki katika maonesho haya ya wiki ya sheria kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu tatizo la dawa za kulevya. Maonesho haya ni fursa muhimu kwetu katika kuelimisha jamii kuhusu makosa ya dawa za kulevya na adhabu zilizoainishwa kwenye Sheria yetu ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya.
Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015 inatoa adhabu kali kwa makosa mbalimbali yanayohusiana na dawa za kulevya, ikiwa ni pamoja na Kumiliki dawa za kulevya, kusafirisha dawa za kulevya, kuzalisha, kutumia n.k adhabu zake zinafikia hadi kifungo cha maisha jela.
Lengo ni kuzuia na kupambana na tatizo la dawa za kulevya kwani matumizi ya dawa za kulevya yanasababisha madhara makubwa kwa jamii, ikiwa ni pamoja na uhalifu, umaskini, magonjwa mbalimbali, uharibifu wa mazingira , uratibu, kuvunjika kwa familia n.k
Hivyo, natoa wito kwa wananchi wa jiji la Dodoma kutembelea banda letu ili kujifunza zaidi kuhusu dawa za kulevya, sheria zinazosimamia dawa za kulevya, na jinsi ya kujilinda dhidi ya dawa za kulevya.
0 Comments