Raisi Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Afariki Dunia.



Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi afariki Dunia leo hii tarehe 29 Februari 2024.

Mzee Mwinyi alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia 30 January 1984 mpaka 24 October 1985, alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 mpaka 1995.

Mzee Mwinyi amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kuanzia mwaka 1990 mpaka 1996.

Rais Mwinyi akiwa Rais wa Tanzania ndipo nchi nyingi barani Afrika ziliingia katika mfumo wa Vyama vingi vya siasa “Multiparty Democracy” hapo ndipo jina la utani la “Mzee Rukhsa” lilipoanza, kwani Serikali ilianza kuruhusu mambo mengi kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania pamoja na kukuza uhusiano na mataifa ya Magharibi.

Rais Mwinyi atakumbukwa kwa Uchapakazi pamoja na ucheshi wake.

Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Mpira na Shule ya Sekondari ya Ali Hassan Mwinyi Tabora, pamoja na Ali Hassan Mwinyi Elite School Jijini Dar es Salaam ni baadhi ya sehemu zilizopewa jina lake ili kuenzi mchango wake katika utawala bora.

Post a Comment

0 Comments