Uwekezaji Mkubwa Wa SERIKALI Mamlaka DCEA Waleta Tija.


Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema imepata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 2023 kilogramu zaidi ya milioni moja za aina mbalimbali za dawa za kulevya zilikamatwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari tarehe 20 Februari 2024 Jijini Dodoma kuhusu taarifa ya mafanikio ya Serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya Mhe. Jenista alisema Watuhumiwa 10,522 walikamatwa ambao kati yao wanaume ni 9,701 na wanawake ni 821 huku akisema kuwa jumla ya hekari 2,924 za mashamba ya bangi na mirungi ziliteketezwa.




“Kiasi cha dawa zilizokamatwa kwa mwaka mmoja ni zaidi ya mara tatu ya dawa za kulevya zilizokamatwa kwa kipindi cha miaka 11 hapa nchini, kwani miaka 11 iliyopita tulifanikiwa kukamata kilogramu 660,465 pekee. Aidha, Serikali imefanikiwa kuzuia uingizaji wa kilogramu 157,738.55 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya kinyume cha sheria,” Alisema Mhe. Jenista.

Waziri Jenista amesema mafanikio ya ukamataji huu yanatokana na nia, utashi na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan. “Mara baada ya kuingia madarakani ameonesha dhamira yake kwa vitendo katika kuiimarisha Mamlaka kwa kuipa vitendea kazi vinavyohusianisha teknolojia ya isasa ya kimkakati katika mapambano, kutoa mafunzo kwa watumishi ndani na nje ya nchi pamoja na uzalendo wa watendaji kwenye Mamlaka”.

Post a Comment

0 Comments