Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wakala wa misitu (TFS) imefanya operesheni katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Iringa, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata jumla ya Kilogramu 54,506.553 za dawa za kulevya za mashambani na viwandani pamoja na kuteketeza ekari 262 za mashamba ya bangi.
Dawa zilizokamatwa ni bangi kilo 54,489.65, mirungi Kilogramu 10.3, heroin gramu 90.93, cocaine gramu 1.98 na Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32). Watuhumiwa 72 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.
Aidha, dawa hii ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao (internet) na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa
hapa za majina bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imebaini uwepo wa mashamba makubwa ya bangi katika hifadhi za misitu ya Ubangu mkoani Shinyanga na Mabatini mkoani Tabora ambapo wahalifu hao wamekata miti katikati ya misitu hiyo na kulima bangi. Kwa ushirikiano tulioupata kutoka kwa wakala wa misitu (TFS) tulifanikiwa kuteketeza mashamba hayo na kuwakamata wahusika.
Tunatoa shukrani zetu kwa wananchi kwa kutoa taarifa sahihi kuhusu wazalishaji na wauzaji wa dawa za kulevya katika maeneo yao na tutaendelea kushirikiana na wadau na jamii kwa ujumla ili kufanikisha operesheni zetu.
0 Comments