Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis Alaani Mashambulizi Ya Israel Huko Gaza.

 


Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ameungana na viongozi wengine wa dunia kulaani mashambulizi ya jeshi la anga la Israel yaliyowauwa wafanyakazi saba wa shirika la misaada la World Central Kitchen la Uhispania katika Ukanda wa Gaza hapo jana. Papa Francis amesema hivi leo kwamba anawaombea ndugu na jamaa wa marehemu hao, ambao waliuawa wakati wakiwa kwenye shughuli za kugawa misaada ya chakula kwa watu wenye uhitaji mkubwa. Mkuu wa jeshi wa Israel amekiri kwamba mauaji hayo yalikuwa kosa kubwa sana. 

Viongozi kadhaa ulimwenguni, akiwemo mshirika mkuu wa Israel, Rais Joe Biden wa Marekani, wameonesha ghadhabu zao kwa mashambulizi hayo. Umoja wa Mataifa unasema kufikia sasa, wafanyakazi 180 wa mashirika ya misaada wameshauawa tangu vita vianze kwenye Ukanda wa Gaza hapo Oktoba 7.

Unadhani dunia inachukuwa hatua za kutosha kuzuwia mauaji dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kibinaadamu kwenye Ukanda wa Gaza?

Post a Comment

0 Comments