Tetemeko Kubwa la Ardhi lenye Ukubwa wa 7.4 Laikumba Taiwan.


Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 7.4 limetokea Nchini Taiwan usiku wa kuamkia leo na kusababisha uharibifu wa majengo na miundombinu mingine huku usalama wa Watu ukiwa hatarini ingawa bado hakuna ripoti za madhara kwa Binadamu hadi sasa.

Tetemeko hilo limetokea umbali wa KM 18 Kusini mwa Jiji la Huallien na linatajwa kuwa tetemeko kubwa lisilo la kawaida kuwahi kukikumba kisiwa hicho ndani ya miaka 25.

Tahadhari ya kutokea kwa Tsunami imetolewa Taiwan pamoja na Kusini mwa Japan muda mfupi baada ya tetemeko hilo.

Tayari ndege za kivita 30 na meli za kijeshi 9 kutoka China zimefika Taiwan kwa ajili ya kutoa msaada, Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema.

Post a Comment

0 Comments