TRA Yakusanya Tsh Tilion 2.49 Mwezi March Sawa Na Ongezeko La Asilimia 6.91%.


Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi imesema katika mwezi March 2024, TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 2.49, sawa na ufanisi wa 97.05% katika lengo la kukusanya kiasi cha Tsh. trilioni 2.56.

“Makusanyo haya ni ongezeko la 6.91% ukilinganisha na kiasi cha Tsh. trilioni 2.32 kilichokusanywa mwezi kama huu katika Mwaka wa Fedha 2022/23”

“Katika kuhakikisha kuwa lengo la makusanyo ya kodi kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 linafikiwa, TRA inapenda kusisitiza Wanachi waendelee kutoa taarifa juu ya vitendo vinayoashiria ukwepaji wa kodi nchini ikiwemo biashara za magendo na uuzwaji wa bidhaa ambazo hazijabandikwa stempu za kielektroniki (ETS)”

“Ikumbukwe kuwa kukithiri kwa vitendo hivi haviathiri makusanyo ya Mapato ya Serikali pekee, bali vinahatarisha afya na usalama wa wananchi kwa bidhaa hizi kuuzwa sokoni wakati hazina viwango vya ubora kwa matumizi ya binadamu, pia Wafanyabiashara wote wanashauriwa kuendelea kutoa risiti za kielektroniki (EFD) zenye viwango sahihi kila wanapouza bidhaa au kutoa huduma”

“TRA inawashukuru na kuwataka Wananchi wote kuendelea kushiriki katika kampeni ya TUWAJIBIKE kwa kudai risiti stahiki za kielektroniki (EFD) zinazobainisha bidhaa na kiasi sahihi kilicholipiwa, Menejimenti ya TRA pamoja na Bodi ya Wakurugenzi inapenda kuwashukuru Walipakodi na Watanzania wote kwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kulipa kodi na kuthamini juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania kuiletea nchi maendeleo. Kwa kuzingatia juhudi hizi, TRA inaendelea kutoa wito kwa Wananchi wote kuendelea kulipa kodi stahiki kwa maendeleo ya Taifa letu”

Post a Comment

0 Comments