Mahakama ya katiba nchini Uganda imetupilia mbali shauri lililowasilishwa Mahakamani kupinga sheria dhidi ya mapenzi kati ya Watu wa jinsia moja na kusisitiza kuwa sheria hiyo inalinda utamaduni na hadhi ya Watu wa Uganda.
DW ( @dw_kiswahili ) imeripoti kwamba Walalamikaji walitaja sababu mbalimbali wakitaka itupiliwe mbali ikiwemo kusema Bunge la Nchi hiyo halikufuata utaratibu stahiki katika kujadili na kupitishwa muswaada wa sheria hiyo na kwamba sheria hiyo ilipitishwa baada ya kujadiliwa kwa siku sita tu badala ya 45 kama inavyotakiwa.
Maamuzi ya mahakama ya katiba yenye kurasa 200 yamesomwa kwa muhtasari na Naibu Jaji Mkuu aitwae Richard Buteera akinukuu dondoo mbalimbali zilizowapelekea kufikia maamuzi hayo ambapo amenukuliwa akisema “tunakataa kutupilia mbali sheria hii kwa sababu kimsingi inalinda hadhi na utamaduni wetu ambao huzingatia familia kuwa taasisi muhimu kukuza jamii”.
Mawakili wa upande wa Walalamikaji wanaojumuisha hasa makundi ya jumuiya ya mapenzi ya jinsia moja maarufu kama LGBTQ wamepinga maamuzi hayo na kuwakosoa Majaji kwa kile wanachokitaja kuwa kujenga hisia za ubaguzi wakisingizia utamaduni na kusisitiza kuwa watawasilisha rufaa Mahakamani kupinga maamuzi hayo.
0 Comments