Waziri Silaa Mabango ya "Viwanja Vinauzwa Hapa" Marufuku.




Waziri mwenye dhamana ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Jerry Silaa, ametoa agizo la katazo la mabango yaliyozagaa mitaani ya kuuza viwanja maarufu viwanja vinauzwa, na kutoa siku 7 kwa Maafisa Ardhi Nchi nzima, kuhakikisha mabango hayo yanaondolewa na kutoa maagizo kwa Makampuni yote yanayouza viwanja, kuweka dawati la mauzo Ofisi za Ardhi za Wilaya na Mikoa.

Mh. Silaa ametoa maagizo hayo katika Ofisi za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi waliofika kutafuta haki zao, baada ya kuuziwa viwanja hewa na Kampuni ya Digital Auction LTD kwenye eneo ambalo hawalimiliki katika Manispaa ya Kigamboni na kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 166.
 

Post a Comment

0 Comments